41
Rap
Tekst piosenki
[Verse 1] - Salmin Swaggz
They say, napenda unavyochana kama Easy E
Wananiuliza mtaani vipi mbona hatusikii
I heard ulianza fanya rap 2003
Mi nna visions, you gotta be blind to see
Niko makini sio beef za kiuswahilini
So snitch...kaa mbali nami mi pesa pesa na mimi
Bila pesa hakuna life...hutaki, kufa maskini
Usiniblame Scandal chafu na matusi ya mwilini
Enzi hizo sikuelewa maisha naispend pesa isokwisha
Wajinga walishindwa bainisha life walitaka ipindisha
Niko...duniani kama sielewi what's going on
Baniani,fanani hatuachani...mabeef, Money n so on
Kwa upeo na hizi akili mi ni dili
So hili pini wanaliafiki wenye roho na wasio na mwili
Mi ndo...sauti ya mtaa...bungeni huu ndo wasaa
Chungeni izo bambataa...tutaachana kwenye mataa, holla!
[Hook] - Chozi
Nimeshaona mbele, now the game is right on
Kuna vikwazo tele, jasho langu halivuji bure
[Repeat]
[Verse 2] - Salmin Swaggz
Si mgeni kwenye Mitaa maskani imetoweka amani mfano wa...
Mtoto wa nyumbani kuitangaza siri ya ndani
Au kwa nchi ya ki-dictator na wapinzani wakiwemo ndani
Fisadi naona unapeta ila usipime huku kitaani
Fani naiendeleza maslahi hayatanipoteza
Daima siwezi teleza mpaka naliona jeneza
Ni ngumu hamuwezi kucheza, kwa waliojaribu kubeza
Walishindwa kunipoteza...kwenye upenyo napenyeza...ah!
Nafkiri mpaka nahisi stanza zinavuja
Watu wanasubiri mfano wa basi linakuja
Wanakejeli una siku mbili, kwanza umeshachuja
Brother ana division 4 na paper imevuja
Usipime kichwa mi siwazi kama nnavyoongea
Mengi yanayokukuta marafiki wanachochea
Kua Misosi, tafuta pa kutokea
Sio pesa, sio simu, sio gari, sio nyumba, safari utapotea
[Hook] - Chozi
Nimeshaona mbele, now the game is right on
Kuna vikwazo tele, jasho langu halivuji bure
[Repeat]
[Verse 3] - Salmin swaggz
Usishangae mi kukushtua yakupasa uzidishe dua
Ukibisha ni sawa na white T-Shirt gizani unaifua
Nakutreat, zaidi ya Piriton na magonjwa ya mafua
Na hii ni kinga, tahadhari na ushauri kabla ya kuugua
Tamaa itakumaliza kama mwanzo hukujua
Au fanya ka kipindupindu kabla ya inzi kutua
Hii ni zaidi ya mama kumtuliza mtoto akikua
Together tutasmama kumkimbiza asiweze kutuua
Waganga walishatabiri na watabiri wakatafsiri
Hakuna atakayebaki tukiendekeza tama za mwili
Dhiki imekithiri maskini hawana muhimili
Wenye akili hawana dili zimebaki waadhiri na sio siri
No maendeleo, ni ukoloni mamboleo
Wanalia sana jimboni ngoja wavikamate vyeo
Bado kuwekwa jikoni kesho wakuite kimeo
Usintazame machoni ka vipi ukapimwe leo…
(Chorus)
(Chozi)
Nimeshaona mbele, now the game is right on
Kuna vikwazo tele, jasho langu halivuji bure
(Outro)
There’s another one, Noma Records
Nicco, Kalulete, Chozi Sebuyu, Salmin
*fade*
Tłumaczenie
Brak
Najnowsze teksty piosenek
Sprawdź teksty piosenek i albumy dodane w ciągu ostatnich 7 dni